99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Iran yasema imepata ujumbe kutoka pande husika za makubaliano ya nyuklia kupitia Qatar

(CRI Online) Januari 30, 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Bw. Hossein Amir-Abdollahian amesema nchi yake imepata ujumbe kutoka pande husika za makubaliano ya nyuklia ya Mwaka 2015 yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) ikiwemo Marekani kupitia Qatar.

Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari pamoja na mwenzake wa Qatar Bw. Mohammed bin Abdulrahman Al Thani baada ya mkutano wao huko Tehran, Bw. Hossein Amir-Abdollahian ameshukuru nia nzuri ya Qatar kusaidia kuzileta karibu pande zote katika hatua za mwisho za kufikia mwafaka kuhusu kurejesha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Waziri wa mambo ya nje wa Qatar amesema, Marekani imetoa ujumbe mfululizo kwa Qatar ili kuwasilishwa kwa Iran, huku akiongeza kuwa ujumbe huo unahusiana na makubaliano ya nyuklia lakini labda siyo wa moja kwa moja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha