

Lugha Nyingine
Viongozi wa nchi mbalimbali duniani watoa salamu za heri kwa Mwaka Mpya wa Sungura wa Jadi wa China
Mapambo yenye umbo la sungura yakionekana kwenye jengo la maduka makubwa ili kukaribisha Mwaka Mpya wa Sungura wa Jadi wa China huko Kuala Lumpur, Malaysia, Januari 7, 2023. (Picha na Chong Voon Chung/Xinhua)
BEIJING - Wakati Mwaka Mpya wa Sungura wa jadi wa China umewadia, viongozi wa nchi mbalimbali duniani wametuma salamu zao za Heri ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kwa nchi ya China, watu wa China na Wachina wa ng'ambo, na kuelezea matumaini yao ya ushirikiano zaidi na China kuelekea maisha bora ya baadaye.
"Kaka na dada zangu kutoka China na kwenye makazi ya Wachina duniani kote: Nawatakia nyote Heri na Ustawi na Neema katika Mwaka Mpya wa Jadi wa Mwaka 2023 kwa kalenda ya kilimo ya China ," Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema katika taarifa iliyotolewa na Ikulu.
"Tunapoingia mwaka mpya, pia tunasherehekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Watu wa China Mwaka 1998," amebainisha na kuongeza kuwa Afrika Kusini itapokea kutoka China zamu ya kuwa mwenyekiti na mwenyeji wa Mkutano ujao wa BRICS.
"Matukio haya hutoa sababu za kutosha za kusherehekea," amesema.
Katika ujumbe wa video uliotolewa siku ya Jumamosi, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa alitoa pongezi zake za dhati kwa niaba ya serikali ya Zimbabwe na watu wake , na kwa niaba yake mwenyewe, akisema kuwa "msimu mpya unatoa fursa ya kuimarisha mafungamano imara ya urafiki na mshikamano." ambayo yapo kati ya nchi zetu mbili na watu."
Katika ujumbe wa video uliotolewa Jumamosi, Rais wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe amewatakia watu wa China na serikali ya China mwaka wa mafanikio wa Sungura.
Katika ujumbe wake uliotumwa Jumapili kwa Rais Xi Jinping wa China, Rais wa Moldova Ibrahim Mohamed Solih amewatakia watu wa China mafanikio, maendeleo, furaha na afya njema.
"Kwa niaba ya watu wetu nakutakia wewe (China na watu wa China) afya njema, bahati nzuri, na mafanikio mengi mapya ya kiuchumi," amesema Waziri Mkuu wa Serbia Ana Brnabic aliposhiriki kwenye sherehe kuu ya kuukaribisha Mwaka wa Sungura iliyofanyika kwenye Ngome ya Kalemegdan huko Belgrade siku ya Jumamosi.
Viongozi wengine waliotoa salamu za mwaka mpya wa sungura wakiwemo pamoja na Mette Frederiksen, waziri mkuu wa Denmark Lucie Milebou Aubusson, Spika wa Bunge la Gabon, Waziri Mkuu wa Papua New Guinea, James Marape, Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Fiji, Sitiveni Rabuka na wengine wengi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma