

Lugha Nyingine
Ndege ya kivita ya Russia yafuatilia na kuishinikiza ndege ya kijeshi ya Ujerumani juu ya Bahari ya Baltic
Picha hii kutoka kwenye kumbukumbu ikionesha ndege ya kivita ya Su-27 (Wizara ya Ulinzi ya Russia)
MOSCOW - Ndege ya kivita ya Russia Jumatatu ilitumia mbinu mbalimbali kuifuatilia na kuishinikiza ndege ya doria ya Ujerumani kwenye Bahari ya Baltic, Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema.
“Idara ya Udhibiti wa Anga ya Russia iligundua uwepo wa kifaa fulani kikikaribia mpaka wa nchi ya Russia juu ya Bahari ya Baltic na ndege ya kivita ya Su-27 iliruka kujibu,” wizara hiyo imesema katika taarifa.
Baada ya kutambua kifaa hicho kuwa ni ndege ya P-3C Orion ya doria ya baharini ya Jeshi la Majini la Ujerumani, marubani wa ndege ya kivita ya Russia waliifuatilia na kuishinikiza ndege hiyo hadi iliporuka kutoka kwenye mpaka wa nchi ya Russia, imesema taarifa hiyo.
Imeongeza kuwa, operesesheni hiyo ya kuifuatilia na kuishinikiza ndege hiyo kuondoka ilifanywa kwa kufuata kwa makini sheria za kimataifa za matumizi ya anga juu ya maji yaliyo katika mipaka isiyomilikiwa na upande wowote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma