Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China azitaka Marekani na Japan kuacha kutafuta kuzuia na kukandamiza China
BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin Jumatatu amezitaka Marekani na Japan kuacha chuki zao za kuizuia na kuikandamiza China, kuacha kuzidisha kujijenga kijeshi kwa hatari na kueneza machafuko duniani.
Wang Wenbin ameyasema hayo baada ya viongozi wa Marekani na Japan kutoa taarifa ya pamoja hivi majuzi, ambao wakidai kuwa eneo la Bahari ya Hindi na Pasifiki linakabiliwa na changamoto zinazoongezeka, ikiwa ni pamoja na vitendo vya China visivyoendana na utaratibu wa kimataifa unaofuata sheria. Pia walisisitiza kujitolea kwao kuimarisha muungano wa Marekani na Japan.
"Mkakati mbaya unaotumiwa kwa pamoja na Japan na Marekani kuchafua Sura ya China, kuingilia masuala ya ndani ya China na kukandamiza maendeleo ya China umejaa hatari na unafiki. Tunaukataa kwa uthabiti na tumewasilisha upingaji mkali," msemaji Wang amewaambia waandishi wa habari kwenye mkutano wa kila siku.
Wang ameeleza kuwa vitendo vya Japan vinawafanya watu kujiuliza kama kweli Japan inajitenga na maendeleo ya amani baada ya vita na kuleta hofu ya hatari inayoongezeka ya historia kujirudia.
"Ujumbe wetu kwa Japan ni kwamba yeyote anayetaka kuweka rehani na kuhatarisha usalama na utulivu wa Eneo la Asia-Pacifiki atakataliwa na kurudishwa nyuma na nchi katika eneo hilo," amesema Wang.
Marekani inapenda kuzungumzia kile kiinachoitwa "utaratibu unaofuata sheria", lakini nayo yenyewe ni nchi ya namba ya kwanza ya kuharibu sheria na utaratibu wa kimataifa, Wang amesema, huku akitaja mazoea ya Marekani kama vile kuvamia nchi nyingine bila sababu, vikwazo vya kiholela na utunishaji misuli katika eneo la Asia-Pacifiki kwa kupeleka meli za kivita na ndege za kijeshi, miongoni mwa mambo mengine.
"Lazima ifahamike kuwa China itaendelea na msimamo thabiti kwenye njia ya ujamaa wenye umaalumu wa China. Hakuna nchi au nguvu inayoweza kurudisha nyuma maendeleo ya China. Tutafanya kile kinachohitajika kutetea kwa uthabiti mamlaka ya nchi yetu, usalama na masilahi ya maendeleo," Wang ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma