

Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kutazama uhusiano wa pande hizo mbili kwa mantiki sahihi
BEIJING – China imeitaka Marekani kuitazama China na uhusiano kati ya China na Marekani kutokana na hali halisi na kwa kufaa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema Jumatano.
Wang aliyasema hayo kwenye mkutano na wanahabari alipotoa maoni kuhusu Baraza la Wawakilishi la Marekani kuunda kamati maalumu ya Bunge inayoilenga China.
Tunatumai wanasiasa husika wa Marekani wataitazama China na uhusiano kati ya China na Marekani kutokana na hali halisi na kwa maono ya kimantiki, kuendelea kuzingatia zaidi maslahi binafsi ya Marekani na maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili, ili kuelekea upande mmoja pamoja na China na kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa msingi wa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma