

Lugha Nyingine
Rais Biden amwalika Rais wa Brazil Lula da Silva kuzuru Marekani kufuatia ghasia kutokea
Luiz Inacio Lula da Silva (kushoto), ambaye amevaa mkanda wa urais, akiwasalimia wafuasi wake mjini Brasilia, Brazili, Januari 1, 2023. (Xinhua/Liu Bin)
WASHINGTON - Rais wa Marekani Joe Biden atamkaribisha mwenzake wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva kufanya ziara nchini Marekani mapema Februari, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumatatu baada ya mawasiliano ya simu kati ya marais hao wawili kufuatia ghasia na mashambulizi makali dhidi ya majengo ya serikali ya Brazil.
Taarifa ya pamoja ilisema, rais Lula da Silva alipokea mwaliko huo wa rais Biden, ziara yake hiyo itafanyika ambayo itakusudiwa kutumika kama fursa kwa viongozi hao wawili kuwa na "mashauriano ya kina juu ya ajenda ya pamoja".
Kwenye mawasiliano hayo ya simu, Biden "alilaani ghasia na mashambulizi dhidi ya taasisi za kidemokrasia na mchakato wa kukabidhiana madaraka kwa amani" ambayo Dunia imeshuhudia huko Brasilia, wakati kundi la wafuasi wa Rais wa zamani Jair Bolsonaro walivamia ikulu ya rais ya Brazil, majengo ya bunge na Mahakama Kuu siku ya Jumapili.
Hadi kufikia Jumatatu, zaidi ya watu 1,000 walikuwa wamekamatwa kuhusika na ghasia hizo, kwa mujibu wa taarifa ya hivi punde ya waziri wa sheria wa Brazil, Flavio Dino.
Picha iliyopigwa Agosti 16, 2022 ikionyesha Ikulu ya Marekani huko Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)
Wafuasi wa Bolsonaro walikuwa wakiandamana kupinga kushindwa kwa rais huyo wa zamani na Lula da Silva katika uchaguzi wa rais wa Oktoba mwaka jana. Bolsonaro hakushiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa mrithi wake Januari 1 na sasa yuko katika Jimbo la Florida nchini Marekani, akiripotiwa kulazwa hospitalini kwa sababu ya "kutohisi vizuri."
Katika mkutano na wanahabari siku ya Jumatatu, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alikataa kuweka wazi aina ya visa ambayo Bolsonaro alitumia kuingia Marekani.
Price amesema, wakati "taasisi za kidemokrasia za Brazil zina uungwaji mkono wetu kikamilifu,", Marekani "bado haijapokea maombi yoyote ya habari au hatua" kutoka Brazili kuhusiana na uchunguzi wa ghasia na mashambulizi ya Jumapili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma