

Lugha Nyingine
Rais wa Russia aliamuru jeshi kusitisha vita kwa siku moja na nusu wakati wa sikukuu ya Krismasi ya Waorthodox
(CRI Online) Januari 06, 2023
Picha ikionesha majengo yanayoharibika huko Kiev, Ukraine, Desemba 31, 2022. Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.
Rais wa Russia Vladimir Putin ameliamuru jeshi la nchi hiyo kusitisha vita na Ukraine kuanzia saa sita usiku wa tarehe 6 kwa saa za Russia hadi saa sita usiku wa tarehe 7, ili kupisha Sikukuu ya Krismasi kwa watu wa dhehebu la Orthodox.
Rais Putin amesema hatua hiyo inafuatia pendekezo lililotolewa na uongozi wa dhehebu hilo nchini Russia. Pia rais Putin ametoa wito kwa Ukraine kusitisha vita ili kuwapa waumini fursa ya kufanya shughuli za kidini wakati wa kipindi cha Krismasi ya Waorthodox.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma