99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Bandari ya Shanghai yaendelea kuwa bandari ya makontena yenye shughuli nyingi zaidi duniani Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2023

Picha iliyopigwa Mei 17, 2022 ikionyesha mwonekano wa kituo cha makontena cha kiotomatiki cha Bandari ya Kina Kirefu ya Yangshan ya Shanghai iliyoko katika Mji wa Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ding Ting)

SHANGHAI – Takwimu zilizotolewa na Bandari zimeonesha kuwa, Bandari ya Shanghai imeendelea kuwa bandari yenye mizigo mingi zaidi duniani kwa mwaka wa 13 mfululizo katika Mwaka 2022, licha ya janga la UVIKO-19.

Takwimu zilizotolewa na Kampuni ya Kimataifa ya Bandari ya Shanghai, ambayo ni mwendeshaji wa bandari hiyo zimeonesha kuwa, makontena yaliyopakiwa na kupakuliwa kutoka bandari yalikuwa zaidi ya milioni 47.3 yenye urefu wa sawa na futi 20 (TEUs) kila moja Mwaka 2022.

Ikikabiliana na janga, pamoja na mawimbi ya joto na baridi mwaka jana, bandari hiyo ilihakikisha utendakazi thabiti wa Kituo cha Kimataifa cha Usafirishaji cha Shanghai na kulinda uthabiti wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi.

Kufuatia milipuko ya hapa na pale ya janga hilo katika robo ya pili ya mwaka huu, bandari hiyo ilifanikiwa kurejesha kwa haraka huduma za makontena mwezi Julai, iliposhughulikia rekodi ya juu ya mwezi ya makontena milioni 4.3.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha