Watu milioni 100 duniani wakimbia makazi yao Mwaka 2022
Shirika la Kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Jumatatu lilisema watu milioni mia moja kote duniani walilazimika kukimbia makazi yao katika mwaka huu wa 2022, wakati huohuo Umoja wa Mataifa unaendelea kusaidia wale wenye mahitaji kwa njia nyingi.
Mkuu wa shirika hilo, Filippo Grandi, ameelezea idadi hiyo kama "rekodi isiyopaswa kuwekwa". Idadi hiyo imeongezeka kutoka watu milioni 90 Mwaka 2021. Kuzuka kwa vurugu, au migogoro ya muda mrefu, ndiyo sababu kuu za watu kukimbia makazi yao katika sehemu nyingi za dunia, ikiwa ni pamoja na Ukraine, Ethiopia, Burkina Faso, Syria na Myanmar.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa maelfu ya wahamiaji waliokata tamaa waliichukulia Ulaya kama eneo lao la kukimbilia, wakiweka maisha yao mikononi mwa wafanya biashara haramu ya binadamu, na kuanza safari za hatari kuvuka bahari ya Mediterania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma