

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine asema Ukraine itafanya mkutano wa kilele wa amani msimu huu wa baridi
KIEV - Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba amesema Kiev inatarajia kufanya mkutano wa kilele kujadili mpango wa amani wa Ukraine ifikapo mwisho wa Februari Mwaka 2023, shirika la habari la Ukraine, Interfax limeripoti Jumatatu.
"Umoja wa Mataifa unaweza kuwa jukwaa bora zaidi la kufanya mkutano huu," Kuleba amesema, huku akipendekeza kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atakuwa mpatanishi anayewezekana wa mazungumzo hayo ya amani.
Kuleba anaamini kuwa Russia haiko tayari kwa mazungumzo ya amani, ingawa waziri huyo amedokeza kuwa "kila vita huisha kutokana na hatua zilizochukuliwa kwenye uwanja wa vita na kwenye meza ya mazungumzo."
Akitoa maoni yake kuhusu ziara ya hivi majuzi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky nchini Marekani, Kuleba amesema "ameridhika kabisa" na matokeo yake.
Zelensky alipendekeza na kutoa mpango wa amani wa kumaliza vita kati ya Russia na Ukraine katika mkutano wa G20 nchini Indonesia mwezi uliopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma