

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na mwenyekiti mwenza wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Asia
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akifanya mazungumzo na John L. Thornton, mwenyekiti mwenza wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Asia, mjini Beijing, China, Desemba 22, 2022. (Xinhua/Zhang Ling)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Alhamisi alikutana na John L. Thornton, mwenyekiti mwenza wa Bodi ya Wadhamini ya Jumuiya ya Asia.
Ili kufikia maendeleo thabiti na endelevu ya uhusiano kati ya China na Marekani, upande wa Marekani unapaswa kwanza kuwa na mtazamo sahihi juu ya China, amesema Wang.
Wang amesema wakuu wa nchi hizo mbili walifikia makubaliano muhimu ya kutafuta namna na kuweka kanuni elekezi za uhusiano wa pande mbili wakati wa mkutano wao huko Bali, kujadili namna ya kufuata njia sahihi ya kutendeana kwa nchi hizo mbili kwa kuzingatia kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.
Upande wa Marekani unapaswa kuachana na uzuiaji wake usio na sababu na ukandamizaji dhidi ya China, kuweka kauli za Rais wa Marekani Biden katika vitendo, na kurejea katika sera na vitendo vyenye hamasa kuhusu China, ameongeza.
Amesema, kutokana na masuala ya kikanda na changamoto zinazojitokeza mara kwa mara duniani kama vile mabadiliko ya tabia nchi na matatizo ya chakula na nishati, China na Marekani zikiwa nchi mbili kubwa zinapaswa kufanya ushirikiano unaohitajika. Hili ni jukumu linalostahili la nchi kubwa, pamoja na matarajio ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa.
Wang amesema, "Tuko tayari kufanya mazungumzo katika ngazi zote na Marekani," China inakaribisha makampuni ya Marekani, na wataalamu wa kimkakati na kitaaluma kuja China kwa mazungumzo zaidi ya ana kwa ana ili kuongeza maelewano kati ya nchi hizo mbili.
Kwa upande wake Thornton amesema Marekani na China zinapaswa kuwa washirika wa kimkakati wanaoweza kushirikiana. Amesema ataendelea kutekeleza jukumu lake katika kukuza biashara na mabadilishano ya kiuchumi kati ya Marekani na China, kuongeza uelewa wa jumla wa Wamarekani kuhusu China, na kuhimiza ukuaji thabiti wa uhusiano wa Marekani na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma