99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kutatuliwa kwa vitendo matatizo ya Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 20, 2022

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wa mwisho wa mwaka kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Desemba 19, 2022. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres siku ya Jumatatu ametoa wito wa kutatuliwa kwa vitendo matatizo ya Dunia licha ya sababu nyingi za kukata tamaa.

"Dunia yetu ilikabiliwa na majaribu na mitihani mingi Mwaka 2022 -- baadhi ni ya kawaida, mengine ambayo hatukuwa tukiyafikiria mwaka mmoja uliopita. Kunaweza kuwa na sababu nyingi za kukata tamaa," ameuambia mkutano na waandishi wa habari wa mwisho wa mwaka kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Mgawanyiko wa siasa za kijiografia umefanya utatuzi wa matatizo duniani kuwa mgumu zaidi -- wakati mwingine kutowezekana. Msukosuko wa gharama za maisha unazidi kudorora na ukosefu wa usawa unaongezeka, na kuathiri zaidi wanawake na mabinti duniani. Nchi nyingi maskini zaidi duniani zinajikuta kwenye kile ambacho mtu anaweza kukiita "msongo wa madeni" -- zikitazama chini kwenye dimbwi la ufilisi na kushindwa kulipa. Mwaka huu pekee malipo yao ya huduma ya madeni yaliongezeka kwa asilimia 35 – ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi katika miongo kadhaa, amesema Guterres.

"Changamoto hizi na nyingine nyingi huwafanya wengine kutaka kunyoosha mikono juu na kuachana na masuala ya kimataifa ya kutatua matatizo na diplomasia. Lakini namaliza mwaka huu kwa imani moja kuu: huu si wakati wa kukaa pembeni, ni wakati wa kusuluhisha, kufanya maamuzi, na – hakika -- hata matumaini, kwa sababu licha ya mapungufu na hali mbaya ya muda mrefu, tunafanya kazi kurudisha nyuma hali ya kukata tamaa, kupigana dhidi ya kukata tamaa na kutafuta suluhisho la kweli," Guterres amesisitiza.

Guterres ameangazia baadhi ya maendeleo, kama vile makubaliano ya Mfumokazi mpya wa Bioanuwai wa Dunia katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai huko Montreal, Canada, na kuimarika kwa baadhi ya migogoro inayoendelea duniani.

Nchini Ethiopia, kusitishwa kwa uhasama na makubaliano ya utekelezaji yapo. Njia ya usaidizi katika sehemu ya Kaskazini mwa nchi inajitokeza. Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, juhudi za kidiplomasia zinazoongozwa na Angola na Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeunda mfumo wa mazungumzo ya kisiasa ili kutatua mgogoro wa eneo la Mashariki mwa nchi hiyo. Usimamishaji wa Mapigano nchini Yemen umeleta manufaa halisi kwa watu. Safari za ndege za abiria zimeanza tena kutoka Sanaa. Vifaa muhimu hatimaye vinapitia bandari ya Hodeidah, ameeleza.

Ameongeza kuwa, licha ya changamoto zinazoendelea, Mpango wa Nafaka wa Bahari Nyeusi wa kuwezesha mauzo ya nje ya chakula na mbolea kutoka Ukraine -- na mkataba wa maelewano wa usafirishaji usiozuiliwa wa chakula na mbolea kutoka Russia kwenye masoko ya kimataifa -- unaleta mabadiliko. Zaidi ya tani milioni 14 za nafaka na vyakula vingine zimesafirishwa kutoka bandari za Bahari Nyeusi nchini Ukraine. Mauzo ya ngano ya Russia pia yameongezeka mara tatu.

Huku akisifu mafanikio hayo, Guterres amesenma Mwaka 2023 utakuwa mwaka wa amani, mwaka wa kuchukua hatua. “Hatuwezi kukubali mambo jinsi yalivyo. Tuna deni kwa watu kutafuta suluhu, kupambana na kuchukua hatua," amesema Guterres.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wa mwisho wa mwaka kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Desemba 19, 2022. (Xinhua/Xie E)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha