99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mfumokazi wa Kimataifa wa Bioanuwai wa Kunming-Montreal wapitishwa katika COP15

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 20, 2022

Huang Runqiu, Mwenyekiti wa COP15 na waziri wa ikolojia na mazingira wa China, akitangaza kupitishwa kwa Mfumokazi wa Bioanuwai wa Kimataifa wa Kunming-Montreal, ambao ni makubaliano ya Umoja wa Mataifa yanayolenga kubadilisha mwelekeo wa upotevu wa viumbe anuwai na kuweka Dunia katika njia ya kurejesha bioanuwai, katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, COP15 huko Montreal, Canada, Desemba 19, 2022. COP15, inayojulikana rasmi kama mkutano wa 15 wa Mkutano wa Nchi Watiasaini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, umehitimishwa jana Jumatatu baada ya karibu wiki mbili za majadiliano. China ikiwa nchi mwenyekiti wa COP15. COP15 ilifanya mkutano wa awamu ya kwanza huko Kunming, Mji Mkuu wa Mkoa wa Yunnan Kusini-Magharibi mwa China, Mwaka 2021. Awamu ya pili ya mkutano wa COP15 huko Montreal, Canada, iliendelea ikiwa ni kaulimbiu isemayo "Ustaarabu wa Ikolojia: Kujenga Mustakabali wa Pamoja wa Viumbe Vyote Duniani." (Xinhua/Lian Yi)

MONTREAL, Canada – Makubaliano ya Umoja wa Mataifa yanayolenga kubadilisha mwelekeo wa upotevu wa viumbe anuwai na kuweka Dunia katika njia ya kurejesha bioanuwai zilizopotea yamepitishwa siku ya Jumatatu katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, COP15, huko Montreal, Canada.

"Maudhui yamepitishwa," Huang Runqiu, mwenyekiti wa COP15 na waziri wa ikolojia na mazingira wa China, alitangaza wakati akipiga siwa yake. Shangwe na vifijo kutoka kwa wajumbe waliokusanyika vilijaa ukumbi wa mkutano.

COP15, ambayo inajulikana rasmi kama mkutano wa 15 wa Mkutano wa Nchi Watiasaini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, umehitimishwa jana Jumatatu baada ya karibu wiki mbili za majadiliano. Makubaliano hayo yaliyopitishwa yanajulikana rasmi kama Mfumokazi wa Bioanuwai wa Dunia wa Kunming-Montreal.

Wadau wamekubaliana kuhusu masuala muhimu, ikiwa ni pamoja na malengo na shabaha, uhamasishaji wa rasilimali na Habari Mfululizo za Kidijitali, au DSI, chini ya mfumo huo. Mfumokazi huo unajumuisha malengo manne na malengo 23 ya kufikiwa ifikapo Mwaka 2030.

Mfumokazi pia unaweka shabaha ya kuongeza mtiririko wa fedha wa kimataifa kutoka nchi zilizoendelea hadi nchi zinazoendelea, hasa nchi zilizoendelea kidogo, nchi za visiwa vidogo zinazoendelea na nchi zilizo na uchumi wa mpito, hadi angalau dola za Kimarekani bilioni 20 kwa mwaka ifikapo Mwaka 2025, na angalau dola za kimarekani bilioni 30 kwa mwaka ifikapo Mwaka 2030.

Pia unataka urejeshaji wa bioanuwai ukamilike au uendelee kwa angalau asilimia 30 ya ardhi iliyoharibiwa, maji ya bara, na mazingira ya pwani na baharini.

Baada ya miaka minne ya juhudi, mchakato huo hatimaye umefikia kikomo, Huang amesema, huku akiongeza kuwa maudhui hayo yaliyopitishwa yataongoza juhudi za pamoja za pande zote kukomesha mwelekeo wa upotevu wa bioanuwai ili kuweka Dunia kwenye njia ya kurejesha bionuwai zilizopotea na kuwanufaisha wanadamu wote.

Akielezea mpango huo kama wa kihistoria, Huang amesema mfumokazi huo umeonyesha maono ya Mwaka 2050 ya "kuishi kwa amani na mazingira ya asili."

China ikiwa nchi mwenyekiti wa COP15. COP15 ilifanya mkutano wa awamu ya kwanza huko Kunming, Mji Mkuu wa Mkoa wa Yunnan Kusini-Magharibi mwa China, Mwaka 2021. Awamu ya pili ya mkutano wa COP15 huko Montreal, Canada, iliendelea ikiwa na kaulimbiu isemayo "Ustaarabu wa Ikolojia: Kujenga Mustakabali wa Pamoja wa Viumbe Vyote Duniani." 

Huang Runqiu (wan nne, kulia), mwenyekiti wa COP15 na waziri wa ikolojia na mazingira wa China, na Elizabeth Maruma Mrema (wa pili, kulia), Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, wakipongezana baada ya kupitishwa kwa Mfumokazi wa Kimataifa wa Bioanuwai wa Kunming-Montreal, makubaliano ya Umoja wa Mataifa yanayolenga kubadilisha mwelekeo wa upotevu wa bioanuwai na kuweka Dunia kwenye njia ya kurejesha bioanuwai zilizopotea katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, COP15, huko Montreal, Canada, Desemba 19, 2022. (Xinhua/Lian Yi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha