99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mwenyekiti wa COP15 afurahishwa na maendeleo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa bioanuwai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2022

Huang Runqiu (kati), Mwenyekiti wa COP15 na waziri wa ikolojia na mazingira wa China, akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Montreal, Canada, Desemba 17, 2022. (Xinhua/Ren Pengfei)

MONTREAL, Canada - "Tumepiga hatua madhubuti kuelekea mafanikio," amesema Huang Runqiu, Mwenyekiti wa COP15 na waziri wa ikolojia na mazingira wa China, Jumamosi baada ya kumalizika kwa majadiliano ya ngazi ya mawaziri ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bioanuwai.

Mkutano wa COP15, ambao unajulikana rasmi kama mkutano wa 15 wa Mkutano wa pande zilizosaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Bioanuwai, umepangwa kuhitimishwa leo Jumatatu kwa kupitishwa kwa mfumo wa kimataifa wa bioanuwai wa baada ya Mwaka 2020.

Alipoulizwa kama majadiliano hayo yanaweza kuhitimishwa na kutoa matokeo kwa wakati, Huang ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba ana matumaini. "Tunaweza kuhitimisha majadiliano kama ilivyopangwa," na "Pande zote zinataka kufikia makubaliano."

"Katika siku mbili zilizopita, tutazingatia masuala machache. Pindi tu mafanikio yanapofanywa kuhusu masuala haya, tunaweza kuwa na mfumo," ameongeza.

Mkutano huo wa mawaziri ulianza Alhamisi na kumalizika Jumamosi asubuhi. Mkutano huo wa siku mbili na nusu umekuwa na jukumu muhimu sana katika kuhimiza mchakato wa mazungumzo ya COP15, amesema Huang.

Amesema mawaziri wameonyesha nia thabiti ya kisiasa ya kubadili upotevu wa viumbe hai duniani na kukiri kuwa mkutano huo ni dirisha la mwisho la fursa ya kufanya mabadiliko hayo.

"Lazima tushindane na wakati, kukabiliana na sababu za upotevu wa viumbe hai, na kuchukua hatua za mageuzi katika uzalishaji, matumizi na biashara," Huang amesema. "Lazima pia tuanzishe mbinu za kisayansi za kupima gharama za asili za shughuli za kiuchumi, kukusanya rasilimali nyingi iwezekanavyo na kuweka utaratibu wa utekelezaji na mipango ya utekelezaji ya kitaifa ili kufanya mfumo kabambe na wa kweli kufanya kazi."

Mawaziri kutoka nchi zilizoendelea na zinazoendelea wamesaidia vikundi kazi kufikia maendeleo katika majadiliano ya ngazi ya juu ya masuala magumu ikiwa ni pamoja na uhamasishaji wa rasilimali na Mpangilio wa Habari za Kidijitali, unaojulikana kwa jina la DSI, amesema Huang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha