

Lugha Nyingine
Balozi wa China na Waziri wa Hazina wa Marekani wakutana kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya viongozi
Balozi wa China nchini Marekani Qin Gang (Kushoto) akipeana mkono na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen kwenye mkutano wao mjini Washington, D.C., Marekani, Desemba 15, 2022. Balozi Qin Gang alikutana na Janet Yellen siku ya Alhamisi na viongozi hao wamejadili utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya marais wa nchi hizo mbili na kuahidi kuendelea kushirikiana. (Xinhua)
WASHINGTON - Ubalozi wa China mjini Washington umesema, Balozi wa China nchini Marekani Qin Gang alikutana na Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen siku ya Alhamisi na viongozi hao wamejadili utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya marais wa nchi hizo mbili na kuahidi kuendelea kushirikiana.
"Pande hizo mbili zilifanya mazungumzo ya kina kuhusu utekelezaji wa makubaliano muhimu ya pamoja ambayo marais wawili wamefikia katika mkutano wao wa Bali pamoja na masuala ya kiuchumi na kifedha ya pande mbili na ya kimataifa ambayo yanafuatiliwa kwa pamoja," ubalozi huo umesema katika taarifa yake.
"Pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea kudumisha ushirikiano, kuimarisha uratibu wa sera za uchumi mkuu na mawasiliano kuhusu masuala ya uchumi na biashara ya pande mbili, kushughulikia kwa pamoja changamoto za kimataifa, na kuhimiza maendeleo yenye ustawi mzuri na utulivu ya uhusiano kati ya China na Marekani," imesema taarifa hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma