99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Malaysia wafanya mazungumzo kuhusu uhusiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2022

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Malaysia Zambry Abdul Kadir kwa njia ya video, Desemba 14, 2022. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Malaysia Zambry Abdul Kadir kwa njia ya video siku ya Jumatano.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema China na Malaysia ni marafiki na washirika wazuri, China iko tayari kushirikiana na serikali mpya ya Malaysia ili kuendeleza urafiki na kuimarisha ushirikiano.

Wang amesema China iko tayari kutumia fursa ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Malaysia Mwaka 2023 na maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Malaysia Mwaka 2024 kufanya juhudi za pamoja kuelekea ujenzi wa Jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja, kusukuma uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwenye ngazi mpya, na kulinda kwa pamoja amani, utulivu na ustawi wa kikanda.

Kwa upande wake Zambry ameipongeza China kwa mafanikio ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Huku akipongeza urafiki wa jadi kati ya watu wa pande hizo mbili na kuheshimiana na kuaminiana kati ya nchi hizo mbili, Zambry amesema serikali mpya ya Malaysia iko tayari kushirikiana na China ili kuimarisha mabadilishano ya hali ya juu na kuzidisha ushirikiano katika sekta mbalimbali.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha