99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Virusi kadhaa vinavyoathiri mfumo wa kupumua "vinaenea kwa pamoja" na mafua huko Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2022

Mtu anaonekana akitembea kukipita kituo cha huduma ya dharura kinachotoa chanjo dhidi ya mafua huko New York, Marekani, Tarehe 7 Desemba 2022. (Picha na Michael Nagle/Xinhua)

LOS ANGELES - Virusi kadhaa vinavyoathiri mfumo wa kupumua kwa sasa vinazunguka pamoja na mafua nchini Marekani, kimesema Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), na kuutaka umma kudungwa chanjo dhidi ya mafua na ya nyongeza dhidi ya UVIKO-19 ili kujikinga dhidi ya kuugua kwa hali ya umahututi.

Maambukizi ya mafua ya msimu yako juu kote nchini Marekani. Hadi kufikia sasa msimu huu, kumekuwa na angalau wagonjwa milioni 13, wagonjwa wa kulazwa hospitalini 120,000 na vifo 7,300 kutokana na mafua, kwa mujibu wa makadirio ya hivi karibuni ya CDC.

Kati ya virusi vya mafua A vilivyogunduliwa na kuainishwa katika wiki ya hivi punde inayoishia Desemba 3, asilimia 76 yamekuwa mafua A (H3N2) na asilimia 24 yamekuwa mafua A (H1N1), kwa mujibu wa CDC.

Mkurugenzi wa CDC Rochelle Walensky amesema kuwa uundaji wa chanjo dhidi ya mafua mwaka huu unaendana vizuri kwa aina za virusi vinavyoenea zaidi na kuzunguka nchini humo.

"Tunaangalia katika muda halisi jinsi tunavyofikiri uoanishaji huo mzuri wa mafua ni kwa virusi vinavyosambaa. Na hivi sasa, habari njema ni kwamba inaonekana ni kuoana kuzuri sana," Walensky amesema.

CDC imehimiza umma kupata chanjo dhidi ya mafua na UVIKO-19 kabla ya mikusanyiko mikubwa ya likizo na hali ya hewa ya baridi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha