

Lugha Nyingine
China yaitaka Marekani kuondoa vikwazo dhidi ya maofisa wake
BEIJING - China imeitaka Marekani kuondoa kile kinachoitwa vikwazo dhidi ya maofisa wa China mara moja, na kuacha kuingilia masuala ya Tibet, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin alisema Jumatatu.
Wang Wenbin aliyasema hayo baada ya Marekani siku ya Ijumaa kuwawekea vikwazo maofisa wawili waandamizi wa China kutokana na kile Marekani ilichokiita ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu katika Mkoa unaojiendesha wa Tibet.
Wang amesema upande wa Marekani umeweka vikwazo visivyo halali kwa maofisa wa China chini ya sheria za Marekani na kisingizio cha kile kinachoitwa masuala ya haki za binadamu huko Tibet, ambayo "inaingilia kwa kiasi kikubwa mambo ya ndani ya China, inakiuka waziwazi kanuni za msingi katika uhusiano wa kimataifa na kuathiri sana uhusiano kati ya China na Marekani."
"China inapinga vikali na inalaani vikali," Wang amesema.
Amesema Marekani haina haki ya kuweka vikwazo visivyo na msingi dhidi ya nchi zingine na haina nafasi ya kujifanya kama "polisi wa Dunia".
Amesema China itachukua hatua stahiki na madhubuti ili kulinda haki na maslahi yake halali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma