Marais Putin na Erdogan wajadili kwa njia ya simu ushirikiano wa nishati na mpango wa kuuza nafaka
Rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
MOSCOW - Rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan wamejadili ushirikiano katika sekta ya nishati na mpango wa kuuza nafaka wa Bahari Nyeusi kwenye mazungumzo ya simu siku ya Jumapili.
Viongozi hao wamesisitiza umuhimu maalum wa miradi ya pamoja ya nishati, haswa katika gesi, na kuendelea kubadilishana maoni juu ya mpango wa Putin wa kuweka kituo cha gesi cha kikanda huko Uturuki, Ikulu ya Russia, Kremlin imesema katika taarifa.
Putin na Erdogan pia wamejadili makubaliano yaliyotiwa saini mjini Istanbul Mwezi Julai kuhusu kusafirisha nafaka za Ukraine kutoka bandari za Bahari Nyeusi na kusambaza bidhaa za kilimo na mbolea za Russia kwenye masoko ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma