

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na Balozi wa Russia nchini China
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akikutana na Balozi mpya wa Russia nchini China Igor Morgulov hapa Beijing, mji mkuu wa China, Novemba 27, 2022. (Xinhua/Yan Yan)
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi Jumapili amekutana na Balozi mpya wa Russia nchini China Igor Morgulov.
Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amemkaribisha balozi huyo kuanza wadhifa wake mpya nchini China, na kuongeza kuwa China na Russia zinashikilia kuhimiza Dunia yenye ncha nyingi na haziamini katika Dunia yenye ncha moja ya ukiritimba wa upande mmoja .
Nchi zote mbili zimejitolea kudumisha mfumo wa kimataifa na Umoja wa Mataifa ukiwa katika msingi wake na utaratibu wa kimataifa unaofuata sheria za kimataifa, na kukataa siasa za mabavu, Wang amesema.
“Haijalishi jinsi hali ya kimataifa inaweza kubadilika, China na Russia zitaendeleza kuaminiana kimkakati na ushirikiano wa kivitendo na kudumisha kwa pamoja usawa na haki ya kimataifa,” amesema.
Kwa upande wake Morgulov amesema uhusiano kati ya Russia na China hauwezi kuvunjika na urafiki kati ya nchi hizo mbili unaweza kushinda changamoto yoyote.
Pande hizo mbili pia zimebadilishana mawazo kuhusu masuala ya kimataifa na ya kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma