99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei ya Marekani yasababisha malalamiko kutoka kwa Ulaya

(CRI Online) Novemba 25, 2022

Rais Joe Biden wa Marekani alisaini Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei mnamo mwezi Agosti mwaka huu, ambayo inaruhusu serikali ya Marekani kutoa ruzuku kubwa kwa viwanda vya magari ya umeme yanayotengenezwa nchini humo, hatua ambayo imesababisha malalamiko kutoka kwa nchi za Umoja wa Ulaya (EU).

Waziri wa Uchumi na Fedha wa Ufaransa Bw. Bruno Le Maire na Naibu Waziri mkuu wa Ujerumani Bw. Habeck wamefanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Paris. Bw. Le Maire amesema serikali za Ufaransa na Ujerumani zimekubaliana kuwa zinapaswa kujibu vikali Sheria ya Kupunguza Mfumuko wa Bei wa Marekani, na EU lazima itetee maslahi yake.

Rais Macron wa Ufaransa amewashawishi wafanyabiashara wa Ulaya waendelee kubaki Ulaya na kuiwekeza Ulaya.

Gazeti la "Financial Times" la Uingereza limesema kwamba hatua ya ruzuku ya Biden ni ishara ya hatari, inayozilazimu nchi za Ulaya kuwa macho.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha