99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Uturuki na Cuba zatia saini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2022

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia) akisalimiana na Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Ankara, Uturuki, Novemba 23, 2022. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumatano kwamba nchi yake inataka kuimarisha ushirikiano na Cuba, na nchi hizo mbili zimetia saini mikataba sita katika nyanja za vyombo vya habari na mawasiliano, utamaduni na diplomasia. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

ANKARA - Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Jumatano kwamba nchi yake inataka kuimarisha ushirikiano na Cuba, na nchi hizo mbili zimetia saini mikataba sita katika nyanja za vyombo vya habari na mawasiliano, utamaduni na diplomasia.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu, Ankara, Erdogan alisema kuwa ziara ya kihistoria ya Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel itakuwa hatua mpya katika uhusiano kati ya Uturuki na Cuba.

"Ninatilia maanani umuhimu wa kuimarisha ushirikiano na mshikamano wetu, haswa na Cuba, mmoja wa washirika wetu wa kimsingi katika kanda," aliongeza.

Viongozi hao wawili wamejadili njia za kuendeleza ushirikiano katika nyanja kama vile nishati, utalii, ujenzi, kilimo, maendeleo, afya na mazingira.

Erdogan amesema vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba vimezuia maendeleo ya biashara kati ya Uturuki na Cuba, lakini pande zote mbili zinataka kuongeza kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili hadi kufikia dola milioni 200 za Marekani.

Kwa upande wake, Diaz-Canel amesema wameona dhamira ya pamoja ya kuendeleza uhusiano wa kisiasa kati ya nchi hizo mbili na kukubaliana kuimarisha mabadilishano hayo kwa kutumia fursa zilizopo.

Kiongozi huyo wa Cuba amesisitiza kuwa uhusiano wa pande mbili umekuwa ukiendelea "kwa misingi ya kuheshimiana" katika historia. 

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (kulia, nyuma) na Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel (kushoto, nyuma) wakihudhuria mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Ankara, Uturuki, Novemba 23, 2022. (Picha na Mustafa Kaya/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha