99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri wa ulinzi wa China atoa hotuba kwenye Mkutano wa 9 wa Mawaziri wa Ulinzi wa ASEAN Plus nchini Cambodia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2022

Waziri wa Ulinzi wa China Wei Fenghe (katikati) akitoa hotuba kwenye Mkutano wa 9 wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN- ADMM-Plus) mjini Siem Reap, Cambodia, Novemba 23, 2022. (Picha na Li Xiaowei/Xinhua)

SIEM REAP, Cambodia - Waziri wa Ulinzi wa China Wei Fenghe Jumatano ametoa hotuba kwenye Mkutano wa 9 wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN-ADMM-Plus) hapa Siem Reap, nchini Cambodia.

Katika hotuba yake, Wei amesema Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ambao umekamilika kwa mafanikio hivi karibuni, uliweka dira nzuri ya kujenga nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote.

Ameongeza kuwa chini ya uongozi wa Kamati Kuu ya CPC ikiwa na Komredi Xi Jinping katika msingi wake, China itajitahidi kuhimiza maendeleo ya kisasa ya China, na lengo la ustawi mkubwa wa Taifa la China hakika litatimia.

Wei amesema kwa sasa amani na maendeleo ya Dunia yanakabiliwa na changamoto kubwa, na kwamba kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja ni chaguo sahihi kwani mustakabali wa Dunia upo ndani yake.

Amesema nchi zote zinapaswa kuungana badala ya kugawanyika, na zinapaswa kuwa zenye usawa badala ya kupindukia, kuwa wazi badala ya kufungwa, na kunufaishana badala ya maslahi binafsi, ili kujenga utaratibu wa kikanda unaoshughulikia matatizo na kukidhi maslahi ya pande zote.

Wei amesema China daima imekuwa ikijitolea kuimarisha utulivu na kutoa nguvu chanya kwa Dunia.

Ameongeza kuwa maendeleo ya amani ya China kwa hakika yatatoa fursa mpya kwa maendeleo ya pamoja ya kimataifa, na kuwa na jukumu la kiujenzi katika kudumisha amani na utulivu wa Dunia.

“Jeshi la China ni jeshi la amani, na linapenda kuendelea kuchangia amani ya Dunia pamoja na majeshi ya nchi nyingine,” Wei amesema, na kuongeza kuwa China haitamani maslahi ya nchi nyingine, bali imesimama kidete kulinda maslahi yake.

Amesema, Jeshi la China linajiamini na lina uwezo wa kuwashinda maadui wote wavamizi.

Huku akieleza kwamba hali ya usalama katika eneo la Asia na Pasifiki bado ni shwari, lakini ikiwa na mambo yanayotia wasiwasi, Wei amesema idara za ulinzi za nchi mbalimbali zinapaswa kudumisha msimamo mkuu wa ASEAN, kutekeleza Pendekeo la Usalama wa Dunia, kufuata ushirikiano wa kivitendo, na kushirikiana kujenga kizuizi imara cha usalama wa kikanda.

Mkutano huo wa 9 wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN-ADMM-Plus) umejadili na kupitisha taarifa ya pamoja kuhusu ushirikiano wa ulinzi ili kuimarisha mshikamano kwa ajili ya usalama ulioanishwa.

Katika mkutano huo, Wei alikutana kwa mfululizo huu na mawaziri wa ulinzi wa nchi kadhaa zikiwemo Marekani, Vietnam, Laos, Australia, New Zealand na Korea Kusini, pamoja na naibu waziri wa ulinzi wa Russia, wakibadilishana mawazo kuhusu kuhimiza ushirikiano wa kijeshi na masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha