99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mawaziri wa Ulinzi wa China na Marekani wafanya mazungumzo kuhusu uhusiano nchini Cambodia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2022

Waziri wa Ulinzi wa China Wei Fenghe (wa pili kulia, mbele), ambaye anahudhuria Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) nchini Cambodia, akifanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin (wa pili kushoto, mbele) huko Cambodia Novemba 22, 2022. (Picha na Li Xiaowei/Xinhua)

SIEM REAP, Cambodia - Waziri wa Ulinzi wa China Wei Fenghe ambaye anahudhuria Mkutano wa Tisa wa Mawaziri wa Ulinzi wa Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini Mashariki (ASEAN) nchini Cambodia, amefanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin huko.

Akimjulisha Austin kuhusu Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, Wei amesema kuwa Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Marekani Joe Biden walifikia makubaliano muhimu wakati wa mazungumzo yao kwenye Mkutano wa 17 wa viongozi wa Kundi la 20 (G20), wakiweka mazingira mazuri ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani.

Wei amesema kuwa inayotakiwa kubeba lawama ni Marekani, siyo China, kwa hali ya sasa ya uhusiano kati ya China na Marekani.

“China inatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na majeshi, lakini upande wa Marekani unapaswa kuheshimu maslahi ya msingi ya China,” amesema waziri huyo wa ulinzi wa China.

Ameeleza matumaini yake kuwa Marekani itatimiza ahadi zake kwenye vitendo, kutekeleza kikweli makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, na kupitisha sera za kimantiki na za kiutendaji kuhusu China ili kurudisha uhusiano wa nchi hizo kwenye njia ya maendeleo yenye hali nzuri na utulivu.

Wei amesisitiza kuwa suala la Taiwan ndilo kiini cha maslahi ya msingi ya China na ni mstari mwekundu wa kwanza usioweza kuvukwa kwenye uhusiano kati ya China na Marekani.

Ameongeza kuwa Taiwan ni Taiwan ya China, na suluhu ya suala la Taiwan ni suala la watu wa China wenyewe na hakuna uingiliaji kutoka nje.

Wei amesema jeshi la China lina nguvu, imani na uwezo wa kulinda kwa uthabiti muungano wa kitaifa.

Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zimetoa maoni kwamba majeshi ya nchi hizo mbili yanapaswa kutekeleza kwa dhati makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu hao wa nchi, kudumisha mawasiliano na mazungumzo, kuimarisha udhibiti na uzuiaji wa migogoro, na kujitahidi kudumisha usalama na utulivu wa kikanda.

Pande hizo mbili pia zimezungumzia kuhusu hali ya kimataifa na kikanda, na kuhusu masuala yakiwemo mgogoro wa Ukraine, Bahari ya China Kusini na Peninsula ya Korea. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha