99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Afisa wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuwepo kwa mbinu za muda mrefu ili kuondoa tishio la uharamia katika Ghuba ya Guinea

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2022
Afisa wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kuwepo kwa mbinu za muda mrefu ili kuondoa tishio la uharamia katika Ghuba ya Guinea
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Martha Ama Akyaa Pobee (mbele) akitoa maelezo kwa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Novemba 22, 2022. "Mtazamo wa jumla na wa muda mrefu" unahitajika ili kushughulikia sababu za msingi na hivyo basi kuondoa kikamilifu tishio la uharamia na ujambazi wa kutumia silaha baharini katika Ghuba ya Guinea, afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema Jumanne. (Loey Felipe/Picha ya UN/Kutumwa Xinhua)

UMOJA WA MATAIFA, - "Mtazamo wa jumla na wa muda mrefu" unahitajika ili kushughulikia sababu za msingi na hivyo basi kuondoa kikamilifu tishio la uharamia na ujambazi wa kutumia silaha baharini katika Ghuba ya Guinea, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Martha Ama Akyaa Pobee amesema Jumanne.

Matukio ya uharamia na ujambazi wa kutumia silaha katika Ghuba ya Guinea yameendelea kupungua, Pobee amekiambia kikao cha Baraza la Usalama wakati akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya uharamia katika eneo hilo. .

Ripoti hiyo imeonesha maendeleo chanya kwani idadi ya matukio ya uharamia na ujambazi wa kutumia silaha katika Ghuba ya Guinea ilipungua kutoka 123 Mwaka 2020 hadi 45 Mwaka 2021. Hali hiyo imeendelea Mwaka 2022, huku jumla ya matukio 16 ya uhalifu wa baharini yakiripotiwa kati ya Januari na Juni.

Hata hivyo, Pobee amedokeza kuwa bado ni mapema mno kufikia hitimisho la uhakika kuhusiana na kupungua huku kwa uhalifu.

Akihusisha kupungua kwa idadi ya matukio ya uhalifu, kulikoanza Aprili 2021, na juhudi za pamoja za mamlaka ya kitaifa kwa msaada wa washirika wa kikanda na kimataifa, Pobee amebainisha kuwa uharamia katika Ghuba ya Guinea umepungua zaidi ya miaka kumi iliyopita.

“Vikundi vya maharamia vinabadilika kuendana na mienendo baharini na katika maeneo ya pwani. Kupungua kwa hivi majuzi kwa matukio ya uharamia kunaweza kwa kiasi fulani kuhusishwa na kuhama kwa mitandao ya wahalifu kwenda kwenye aina nyingine za uhalifu wa baharini na mito, kama vile kuchimba mafuta na wizi, ambao wanauona wenye hatari kidogo na faida zaidi,” amesema.

Pobee ametoa wito wa kufanya juhudi kubwa zaidi za kuweka mazingira tulivu na salama ya baharini katika Ghuba ya Guinea.

"Wakati huo huo, sababu za msingi, kama vile ukosefu wa ajira kwa vijana na ukosefu wa huduma za umma, ambazo zinafanya jamii za pwani kuwa katika hatari ya kuingizwa katika vitendo haramu na uhalifu lazima pia kushughulikiwa," amesema.

Pobee amesisitiza kuwa ili kutokomeza kabisa tishio la uharamia katika Ghuba ya Guinea, wadau wa kitaifa, miundo ya kikanda na jumuiya ya kimataifa inapaswa kushirikiana kwa karibu ili kukabiliana na changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira ambazo zinasaidia kuajiri watu binafsi kwenye mitandao ya uhalifu wa baharini.

“Hili linahitaji mtazamo wa ujumla na wa muda mrefu, kwa mujibu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030 ili kukabiliana na umaskini na ukosefu wa njia mbadala za kujikimu, ukosefu wa ajira kwa vijana na ajira za chini ya kiwango,” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha