

Lugha Nyingine
WHO yasema Uganda itapata chanjo za majaribio za homa ya Ebola wiki ijayo
(CRI Online) Novemba 18, 2022
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Uganda itapata chanjo za majaribio ya homa ya Ebola wiki ijayo, wakati nchi hiyo inajitahidi kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo.
Mwakilishi wa WHO nchini Uganda Yonas Tegegn Woldemariam ametoa taarifa akisema kundi la kwanza la watu watakaopata chanjo ni wale waliokutana kwa ukaribu na wagonjwa waliothibitishwa kuambukizwa homa ya Ebola na wahudumu wa afya wanaotibu wagonjwa.
Ameongeza kuwa watu hao lazima waambiwe manufaa na madhara yanayoweza kutokea.
Ofisa anayeshughulikia mlipuko wa homa ya Ebola katika wizara ya afya ya Uganda Henry Kyobe amesema chanjo hizo zimefanyiwa majaribio hapo awali na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa binadamu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma