Makamu wa Rais wa China asisitiza mwendelezo wa sera ili kutoa uhakika na utulivu kwa Dunia
Makamu wa Rais wa China Wang Qishan akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Uchumi Mpya la Bloomberg lililofanyika nchini Singapore kupitia njia ya video Novemba 15, 2022. (Xinhua/Wang Ye)
BEIJING - Makamu wa Rais wa China Wang Qishan amesema Jumanne kwamba sera kuu za Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Serikali ya China zitaendelea kuwa thabiti, na hii itatoa uhakika na utulivu zaidi kwa Dunia.
Wang aliyasema hayo kupitia njia ya video katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Jukwaa la Uchumi Mpya la Bloomberg lililofanyika nchini Singapore.
Katika hotuba yake, Wang ametoa wito kwa nchi kukumbatia maono ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja wakati ambapo amani na maendeleo ya kimataifa yakikabiliwa na hali ya kutokuwa na uhakika inayoongezeka.
“Nchi zinapaswa kushirikiana pamoja ili kuhakikisha usalama wa pamoja, kufuata manufaa ya pande zote na kuendeleza uvumbuzi,” amesema.
Wang ametoa wito wa kutekeleza Pendekezo la Usalama wa Dunia ili kupunguza nakisi ya amani na usalama, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kiwango cha juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuendeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, kuhakikisha utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, na kutafuta njia mpya kwa maendeleo ya kimataifa.
Wang amesema, Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC ulichagua uongozi mkuu mpya wa CPC huku Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC akiwa kiongozi wake, na kusisitiza kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China kupitia njia ya Maendeleo ya Kisasa ya China.
Amesema China itajitahidi kuleta ustawi wa pamoja, kuendelea kuzidisha kufungua mlango wa kiwango cha juu, na kuendelea kujitolea katika njia ya maendeleo ya amani.
“Nchi itashikilia utandawazi wa kiuchumi na kukuza uchumi wa Dunia ulio wa kufungua mlango unaoleta manufaa kwa watu wote ,” amesema Wang.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma