

Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa wasema idadi ya watu wa dunia yafikia bilioni 8
(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, idadi ya watu wa dunia imefikia bilioni 8 tarehe 15, Novemba, 2022.
Kipindi cha “Siku ya idadi ya watu ya bilioni 8” kwenye tovuti ya Umoja wa Mataifa kinajulisha kuwa, huu ni mnara katika historia ya maendeleo ya binadamu. Kuongezeka kwa idadi ya watu wa dunia kunatokana na kuongezeka siku hadi siku kwa miaka ya kuishi kwa watu kwa sababu ya uboreshaji wa huduma ya afya ya umma, chakula bora, hali ya usafi wa binafsi na matibabu. Licha ya hayo, kiwango cha juu cha uzazi cha baadhi ya nchi pia kimehimiza ongezeko la kasi la idadi ya watu.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema, huu ni wakati wa binadamu kufikiria kubeba jukumu la pamoja kwa dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma