

Lugha Nyingine
Kombe la Dunia la Qatar 2022 lawa mchezo ghali zaidi wa FIFA katika historia
Watu wakipiga picha pamoja na bango la Kombe la Dunia la FIFA 2022 kwenye barabara ya Doha Corniche huko Doha, Qatar tarehe 11, Novemba, 2022. (Xinhua)
Kombe la Dunia la Qatar 2022 ambalo limeanzia mwezi Novemba litakuwa mchezo ghali zaidi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) katika historia, ambalo gharama yake ya jumla itakuwa Dola za Marekani bilioni 220 hivi.
Gharama hiyo ni ya juu ikilinganishwa na Kombe la Dunia la Brazil 2014, ambalo lilitumia Dola za Marekani bilioni 11.5 hivi, na Kombe la Dunia la Russia 2018, ambalo gharama yake ilikuwa Dola za Marekani bilioni 14.0 hivi.
Tangu mwaka 2010 Qatar ilipopata nafasi ya kuwa mwenyeji wa kuandaa mchezo wa Kombe la Dunia, siku zote imekuwa ikipanga kwa makini mtandao wa miundombinu, ili kuhudumia mchezo huo wa soka wa kidunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma