Mlipuko mbaya wa shambulizi la kigaidi watokea mjini Istanbul
(CRI Online) Novemba 14, 2022
Makamu wa Rais wa Uturuki Bw. Fuat Oktay amesema kuwa mlipuko uliotokea katika barabara maarufu ya waenda kwa miguu mjini Istanbul umesababisha vifo vya watu sita na wengine 81 kujeruhiwa.
Amesema wanatathmini na kuona kuwa hiki ni kitendo cha kigaidi kilichofanywa na mshambuliaji mwanamke, na kusisitiza kuwa watawakamata wahusika wote, hata wakikimbia hadi ncha ya dunia.
Miongoni mwa majeruhi hao 81 kuna wawili ambao wako katika hali ya mahututi.
Vyombo vya kusimamia utekelezaji wa sheria viko katika hali ya tahadhari, na maafisa wa polisi wanalinda maeneo muhimu huku helikopta zikishika doria katika jiji hilo. Waendesha mashtaka watano wamepewa jukumu la kuchunguza mlipuko huo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma