

Lugha Nyingine
Waziri Mkuu wa China akutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kimataifa na mabadiliko ya tabianchi
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mjini Phnom Penh, Cambodia, Novemba 13, 2022. (Xinhua/Huang Jingwen)
PHNOM PENH - Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres hapa Jumapili kujadili masuala mbalimbali yakiwemo ya uhusiano wa pande nyingi na mabadiliko ya tabianchi.
Li amesema Umoja wa Mataifa ndiyo taasisi kuu ya kudumisha umoja wa pande nyingi. Na kwamba China inatilia maanani sana jukumu muhimu la Umoja wa Mataifa katika kulinda amani ya Dunia na kuhimiza maendeleo ya pamoja.
“Kinyume na hali ilivyo sasa ya kimataifa yenye utata na isiyoeleweka, kushikilia msimamo wa pande nyingi kimsingi kunamaanisha kulinda madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, na kuunga mkono mamlaka ya Umoja wa Mataifa katika kushughulikia masuala ya kimataifa,” Li amebainisha.
Kuunga mkono Umoja wa Mataifa kunatoa mchango kwa amani na maendeleo duniani, Waziri Mkuu wa China Li amesema, huku akiongeza kuwa China inapongeza mafanikio mapya ya Umoja wa Mataifa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Guterres.
Ameahidi kuwa China, kama kawaida, itaimarisha ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa, kuunga mkono na kushiriki kikamilifu katika njia zote za juhudi za Umoja wa Mataifa, na kulinda kwa pamoja madhumuni na kanuni za Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kanuni za sheria za kimataifa na haki na usawa wa kimataifa kwa pande zote.
“Umaskini bila shaka unadhoofisha utulivu, na ni vigumu kuepuka migogoro na machafuko bila kupunguza pengo kati ya Kaskazini na Kusini,” amesema Li.
Li amesema China inaupongeza Umoja wa Mataifa kwa kuyapa kipaumbele masuala ya maendeleo yanayozikabili nchi zinazoendelea na kuzisaidia kikamilifu kupunguza mzigo wa madeni, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kuboresha hali ya maisha, na kutafuta maendeleo endelevu.
Amesema, China ikiwa mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na nchi kubwa zaidi inayoendelea, iko tayari kudumisha mawasiliano na uratibu wa karibu na Umoja wa Mataifa, kufanya kila iwezalo kusaidia nchi zinazoendelea juu ya mabadiliko ya tabianchi chini ya mfumo wa ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kutekeleza jukumu lake la kiujenzi katika kuondoa mzigo wa madeni kwa Afrika chini ya Kundi la Nchi 20 duniani (G20).
Kwa upande wake, Guterres amesema ushirikiano kati ya China na Umoja wa Mataifa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa pande nyingi. Na kwamba Umoja wa Mataifa unathamini juhudi kubwa za China katika kuhimiza ushirikiano wa pande nyingi, na inasifu mchango wa China katika kuendeleza ajenda za Umoja wa Mataifa za kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na kufikia maendeleo endelevu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma