Ajali ya Ndege kugongana na kuanguka kwenye maonesho ya ndege Marekani yasababisha vifo vya watu 6
Daktari wa mahakama wa Jimbo la Dallas huko Texas, Marekani, alitoa ripoti tarehe 13 kwamba watu sita walikufa katika ajali ya ndege kwenye maonyesho ya ndege ya "Mabawa ya Dallas" tarehe 12.
Mchana wa Tarehe 12, ndege mbili zilizotumika kwenye Vita vya Pili vya Dunia zilipofanya maonesho ziligongana na kuanguka haraka na kulipuka, na kusababisha moto mkubwa. Idara ya Usafari wa Ndege ya Marekani ilitoa taarifa ikisema kuwa ndege zilizoanguka zilikuwa ndege ya upigaji mabomu ya B-17 na ndege ya kivita P-63.
Idara ya zimamoto na uokoaji ya Dallas ilisema kwenye mitandao yao ya kijamii kwamba hakukuwa na majeruhi na kifo cha mtu kwenye uwanja wa maonesho.
Maonyesho ya ndege ya "Mabawa ya Dallas" yamekuwa na historia ya miaka saba, ndege 40 za kipindi cha Vita vya Pili vya Dunia zilizooneshwa safari hii, waendeshaji wengi ni marubani waliostaafu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma