99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Ujumbe wa China kwenye COP27 wasema kuhimili kikamilifu mabadiliko ya tabianchi ni kazi ya "halisi na dharura"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 11, 2022

Zhao Yingmin (mbele kwenye mimbari), kiongozi wa ujumbe wa China kwenye Mkutano wa Nchi watia saini wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ikolojia na Mazingira wa China, akizungumza kwenye shughuli ya pembezoni yenye mada ya "Mikakati na Hatua za China katika Kukabiliana na Tabianchi" huko Sharm El-Sheikh, Misri, Novemba 10, 2022. Kukabiliana kikamilifu na mabadiliko ya tabianchi ni kazi "halisi na ya dharura," kiongozi wa ujumbe wa China kwenye mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa amesema siku ya Alhamisi. (Xinhua/Sui Xiankai)

SHARM EL-SHEIKH, Misri - Kuhimili kikamilifu mabadiliko ya tabianchi ni kazi "halisi na dharura," Zhao Yingmin, kiongozi wa ujumbe wa China kwenye Mkutano wa Nchi watia saini wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) amesema siku ya Alhamisi.

Zhao ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ikolojia na Mazingira wa China, ameyasema hayo kwenye shughuli ya pembezoni mwa COP27 yenye mada ya "Mikakati na Hatua za China katika kukabiliana na tabianchi" kwenye mkutano huo wa COP27 unaofanyika katika mji wa pwani wa Sharm El-Sheikh, nchini Misri.

Waziri huyo amesema kuwa kupunguza na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi ndiyo suluhu kuu mbili za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambazo zinapaswa kuzingatiwa kwa usawa na hakuna kati ya hizo inayopaswa kupuuzwa.

“Kwa kuwa mabadiliko ya tabianchi duniani tayari yametokea, hatua madhubuti za kuhimili na kukabiliana na hali hiyo zinaweza kupunguza athari zake mbaya na hatari zinazokabili nchi na kanda ili kulinda maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na usalama wa kiikolojia na mazingira,” Zhao amesema.

Amesema, mbali na kuhimiza uhimilivu na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini, China pia inatekeleza kikamilifu ushirikiano wa Kusini na Kusini na nchi zinazoendelea katika kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.

"China imetoa vifaa kwa nchi zinazoendelea kama vile satelaiti ndogo ndogo, vituo vya kuhamishika vya hali ya hewa, na droni ili kuzisaidia kwenye kuboresha uwezo wao katika masuala ya ufuatiliaji wa majanga ya asili na tahadhari za mapema, pamoja na uwezo wa kuhimili tabianchi," Zhao amebainisha.

Amezitaka nchi zilizoendelea kutimiza ahadi yao ya kutoa dola za Kimarekani bilioni 100 kwa nchi zinazoendelea katika ufadhili wa tabianchi kwa mwaka, na kuweka dira ya kuongeza mara mbili mfuko wa kuhimili tabianchi.

Kuhusu suala la hasara na uharibifu unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, Zhao amesema kuwa ni wasiwasi mkubwa kwa nchi zinazoendelea. "China pia itafanya juhudi na mchango chanya katika kuhimiza maendeleo ya mazungumzo kuhusu hasara na uharibifu," amesema.

Ikiwa imeandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya China, Benki ya Maendeleo ya Asia na Kituo cha Kimataifa cha Kuwezesha Kuhimili Tabianchi, shughuli hiyo ya pembezoni mwa COP27 ilikuwa na majadiliano juu ya sera na hatua zinazohitajika kuchukuliwa ili kukabiliana na kuhimili mabadiliko ya tabianchi, na kubadilishana uzoefu na kesi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha