99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi COP27 waanzisha ajenda ya kusaidia jamii zilizo katika mazingira magumu ya tabianchi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 10, 2022

SHARM EL-SHEIKH - Mkutano unaoendelea wa Nchi watia saini wa Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) siku ya Jumanne ulitangaza kuanzisha ajenda ya "kuimarisha uhimilivu kwa watu bilioni 4 wanaoishi katika jamii zilizo katika mazingira magumu zaidi ya tabianchi ifikapo Mwaka 2030."

Ajenda ya Uhimilivu wa Kukabiliana na Tabianchi ya Sharm-El-Sheikh ilitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry kwenye hotuba katika mkutano wa majadiliano uliofanyika katika mji wa mapumziko wa Bahari Nyekundu wa Sharm El-Sheikh, pembezoni mwa COP27.

Shoukry, ambaye pia ni Mwenyekiti wa COP27, amesema ajenda hiyo ni mpango unaotoa suluhu kwa changamoto za ufadhili na uwekezaji kwenye tabianchi na utekelezaji wa ahadi.

Kwenye taarifa iliyoandikwa, Ofisi ya Mwenyekiti wa COP27 imesema ajenda hiyo inaelezea matokeo 30 ya Uhimilivu wa Kukabiliana na Tabianchi, ambayo kila moja ilitoa suluhu ambazo zinaweza kupitishwa katika ngazi ya nchi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa pamoja, matokeo haya yanawakilisha "mpango wa kwanza wa kina wa kimataifa wa kukusanya watendaji wa serikali na wasio wa serikali nyuma ya seti ya pamoja ya hatua za kukabiliana na tabianchi ambazo zinahitajika kufikia mwisho wa muongo huu katika mifumo mitano ya athari: chakula na kilimo, maji na mazingira ya asili, pwani na bahari, makazi ya watu, na miundombinu, na ikiwa ni pamoja na kuwezesha ufumbuzi wa mipango na ufadhili wa kifedha," imeongeza.

Ajenda hiyo inajumuisha malengo ya kimataifa ya Mwaka 2030 yanayohusiana na mageuzi ya kilimo kinachohimili tabianchi na kilimo endelevu, kulinda na kurejesha mifumo muhimu ya ikolojia, kuweka mifumo ya tahadhari na ya mapema ambayo inaweza kunufaisha karibu watu bilioni 3 kote duniani, uwekezaji katika kulinda mikoko, na kupanua ufikiaji wa watu wa nishati safi ya kupikia, kati ya mengine.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha