99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri wa mambo ya nje wa China akutana na mwenyekiti wa UNGA

(CRI Online) Novemba 09, 2022

(Picha inatoka Shirika la Habari la China Xinhua.)

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana alifanya mazungumzo kwa njia ya video na mwenyekiti wa Baraza Kuu la 77 la Umoja wa Mataifa (UNGA) Bw. Csaba Korosi.

Bw. Wang Yi alisema China siku zote inaunga mkono kazi za Umoja wa Mataifa na jukumu muhimu la UNGA, na itaendelea kushiriki katika ushirikiano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi na kutoa mchango chanya kwa mafanikio ya mkutano wa COP27. Pia amesema China iko tayari kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika sekta ya raslimali za maji pamoja na nchi nyingine kupitia utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo Duniani.

Bw. Korosi amepongeza kufanyika kwa mafanikio kwa mkutano wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China, na kutarajia kuimarisha ushirikiano na China kufanikisha mkutano wa COP27.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha