99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuhimiza usimamizi wa tabianchi duniani

(CRI Online) Novemba 09, 2022

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Kiongozi wa ujumbe wa China kwenye Mkutano wa 27 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP27) Bw. Zhao Yingmin, amesema China inapenda kufanya kazi pamoja na jumuiya ya kimataifa kuhimiza utekelezaji wa pande zote, wenye uwiano na ufanisi wa Makubaliano ya Paris.

Akizungumzia ripoti kuhusu tabianchi na maendeleo nchini China iliyotolewa na Benki ya Dunia, Bw. Zhao Yingmin ambaye pia ni naibu waziri wa ikolojia na mazingira wa China, amesema China imetekeleza mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni changamoto na msukosuko wa pamoja unaowakabili binadamu, na siku zote imekuwa ikifuata kithabiti njia ya kutoa kipaumbele katika uhifadhi wa ikolojia na maendeleo ya kijani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha