99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yashuhudia maendeleo mazuri katika uhifadhi wa ardhi oevu kwa maendeleo ya kiwango cha juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 07, 2022

WUHAN/GENEVA - Katika kisiwa cha katikati ya ziwa katikati mwa Mji wa Wuhan nchini China, zaidi ya ndege mnandi 100 wamejaa kwenye miti 10 ya misonobari. Kwa mwezi mmoja, wataleta kivutio cha rangi nyeupe kama ya theluji kwenye kisiwa hicho hata wakati wa siku ya jua, isiyo na theluji.

"Kuna ndege wengi wanaohamia hapa kiasi kwamba kinyesi chao kitapaka miti rangi kana kwamba imefunikwa na theluji," anasema Shi Chenglu, kiongozi katika Eneo la Maeneo ya Ziwa Mashariki katika Mji wa Wuhan. "Watazamaji wengi wa ndege na wakazi wa kawaida watakuja kufurahia mandhari kutoka kando ya ziwa (bila kutua kwenye kisiwa)."

"Ndege wengi wapya sasa wanaonekana, ikiwa ni pamoja na flamingo wakubwa ambao hatujawahi kuona hapo awali na wari wa Dalmatian ambao hawajatutembelea kwa miaka sita," Wei Bin, makamu mkuu wa jumuiya ya kuangalia ndege ya Wuhan amesema.

Picha iliyopigwa kutoka angani Tarehe 19 Julai 2020 ikionyesha eneo la ardhi oevu la Mto Buh kwenye Ziwa Qinghai, Mkoa wa Qinghai nchini China. (Picha na Yang Tao/Xinhua)

China inapoangazia maelewano kati ya binadamu na mazingira asilia kwenye safari yake kuelekea maendeleo ya kisasa, mito na maziwa mengi katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani yamepokea uwekezaji wa serikali na msaada wa kisheria ambao unaisaidia kurejesha uhai na hata kupanuka zaidi.

Mwaka 1992 China ilitia saini Mkataba wa Ramsar, mkataba ambao ni makubaliano ya kiserikali yaliyowekwa kwa lengo la kufanya juhudi za uhifadhi na matumizi ya busara ya mifumo ya ikolojia ya ardhi oevu.

Tangu wakati huo, China imeanzisha mfumo wa kisheria wa uhifadhi wa ardhi oevu na kutoa mfululizo wa sera za kuongeza ulinzi. Katika muongo uliopita, China imeongeza au kurejesha zaidi ya hekta 800,000 za ardhi oevu, kwa mujibu wa Idara ya Taifa ya Misitu na Uoto asilia ya China.

Akihutubia kwa njia ya video hafla ya ufunguzi ya Mkutano wa 14 wa Nchi Wanachama zilizotia saini Mkataba wa Ramsar kuhusu Ardhi oevu (COP14) huko Wuhan wikiendi iliyopita, Rais wa China Xi Jinping amesema China itahimiza maendeleo ya kiwango cha juu katika suala la uhifadhi wa ardhi oevu.

Wakazi wakifurahia muda wao wa mapumziko katika Hifadhi ya Ardhi Oevu ya OCT Eco huko Wuhan, mji mkuu wa Mkoa wa Hubei, nchini China, Novemba 3, 2022. (Xinhua/Cheng Min)

Ardhi oevu ni pamoja na vyanzo vya maji asilia kwenye nchi kavu, kama vile mito, maziwa, vinamasi, mashamba ya mpunga, pamoja na baadhi ya maeneo ya pwani. Yakijulikana kama "figo za Dunia" na hifadhi ya viumbe hai, maeneo haya ya ardhi oevu yanaweza kusafisha maji na kutoa chakula na makazi kwa ndege wanaohama. Ni miongoni mwa vihifadhi kaboni duniani, ambavyo kuwepo kwao kunachangia juhudi za kimataifa za kupunguza utoaji wa kaboni.

“China itaendelea kutilia maanani ulinzi wa ardhi oevu katika ngazi ya kitaifa na itashusha uwajibikaji ngazi ya chini ili kutekelezwa na serikali za mitaa na vitendo vya kila raia,” amesema Wang Xiangchun, mtafiti kutoka Taasisi ya Utafiti na Usanifu wa Ujenzi wa Miji ya China.

Picha hii iliyopigwa Oktoba 31, 2022 ikionyesha mandhari ya Bustani ya Qingshan huko Wuhan, mji mkuu wa Mkoa wa Hubei katikati mwa China. (Xinhua/Cheng Min)

Kuunganisha ardhi oevu na maendeleo ya kisasa ya China

Licha ya changamoto, miji mingi ya China imesimulia hadithi za mafanikio ya kuunganisha maeneo ya ardhi oevu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Wuhan, ambao ni mji mkubwa wenye wakazi zaidi ya milioni 13 wa kudumu, ni mfano bora. Ukiwa umepewa jina la "mji wa maziwa," Wuhan ni chimbuko la maziwa 166 na umepata mafanikio makubwa katika uhifadhi na uendelezaji wa maeneo ya ardhi oevu.

Miji karibu yote nchini China, sasa imeweka mikakati, sera na sheria za mitaa ambazo huhimiza na kusimamia maendeleo ya uanzishaji na uhifadhi wa ardhi oevu na kuunganisha na maendeleo ya kisasa ya Wachina. 

Watu wakiendesha baiskeli kwenye bustani ya ardhi oevu katika Wilaya ya Liangping, Chongqing, Kusini-Magharibi mwa China, Machi 13, 2021. (Picha na Liu Hui/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha