Wanafunzi wageni wanaosoma China wajikita katika kujifunza teknolojia za kisasa za kilimo
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China wakifanya utafiti hali ya ukuaji wa mahindi kwenye kituo cha majaribio huko Handan, Mkoa wa Hebei wa China. (ChinaDaily/Hu Haijun)
Wanafunzi kutoka Malawi Samson pamoja na wenzake watatu walikwenda kituo cha majaribio kushiriki kwenye shughuli za kilimo huko Handan, Mkoa wa Hebei wa China tarehe 20, Oktoba.
Wao ni wanafunzi wa uzamili wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China wanaosoma Ulinzi wa Mimea na Sayansi ya Maliasili na Mazingira ya asili
Samson mwenye umri wa miaka 30, anatarajia kutumia teknolojia alizojifunza hapa China kusaidia uzalishaji wa kilimo wa taifa lake.
“Kilimo cha China ni cha kisasa sana, na utoaji wa chakula ni mkubwa, kama nitaweza kurudi nyumbani pamoja na teknolojia na maarifa, nazo zitasaidia sana uzalishaji wa kilimo wa nchi yetu,” alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma