

Lugha Nyingine
Watalii nchini China wazidi milioni 73 wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mbalamwezi ya jadi ya China
Picha iliyopigwa Septemba 10 ikionesha watalii wakipanda ngamia wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mbalamwezi ya jadi ya China katika eneo la vivutio la Ziwa la Yueya la Mlima Mingsha la Mji wa Dunhuang, Mkoa wa Gansu wa Kaskazini Magharibi mwa China. (Zhang Xiaoliang/Xinhua)
Takwimu kutoka Wizara ya Utamaduni na Utalii zinaonesha kuwa, idadi ya watalii nchini China ilifikia milioni 73.41 katika likizo ya siku tatu ya Sikukuu ya Mbalamwezi ya jadi ya China kuanzia Jumamosi iliyopita hadi Jumatatu ya wiki hii.
Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, mapato ya jumla ya shughuli za utalii nchini China katika kipindi hicho yalikuwa Yuan bilioni 28.68 (takriban Dola za Marekani bilioni 4.14).
Matembezi wakati wa usiku ni kimoja cha vivutio vya sikukuu hiyo, maziwa na mito ya Hangzhou, Guangzhou, Shanghai na Nanjing na miji nyingine yote ni sehemu zinazowapokea watalii wengi zaidi wakati wa usiku.
Sikukuu ya Mbalamwezi ya jadi ya China ya mwaka huu ilikuwa Jumamosi ya wiki iliyopita. Katika sikukuu hiyo watu wa familia moja moja hujumuika pamoja, kufurahia mbalamwezi na kula keki yenye umbo la mviringo kama mbalamwezi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma