Chongqing yachukua hatua za kubana matumizi ya umeme chini ya wimbi la joto
Picha iliyopigwa Agosti 23 ikionesha hali ya mtaa wa biashara wakati wa usiku mjini Chongqing, China. (Picha/Xinhua)
Kutokana na ukosefu wa umeme uliosababishwa na wimbi la joto linalodumu, vituo kadhaa vya maduka mjini Chongqing, China vimerekebisha ratiba ya kazi — kuwa ya kuanzia saa 10 mchana hadi saa 3 usiku kwa saa za Beijing.
Uarifu uliotolewa na Tume ya Uchumi na Habari ya Chongqing Jumapili ulisema, siku hizi wimbi la joto na moto wa milimani vimesababisha kukatika kwa umeme. Vituo vingi vya maduka vimehusishwa kwenye mpango wa kubana matumizi ya umeme ili kuhakikisha matumizi ya umeme ya wakazi nyumbani.
Uarifu huo ulisema, wakati wa kurudi kwenye hali ya kawaida utatangazwa kutokana na halijoto na uwezo wa utoaji wa umeme.
Habari kutoka tawi la Chongqing la Kampuni ya Mtandao wa Umeme ya China zilisema, matumizi ya umeme ya wakati wa kilele mjini Chongqing yamefikia kiwango cha juu zaidi katika historia.
Mji wa Chongqing umechukua hatua nyingi za kubana matumizi ya umeme kwa ajili ya kulitatua tatizo hilo. Kwa mfano, kwenye vituo na mabehewa ya sabwe taa nyingi zimezimwa, na wakazi wanashauriwa kubana matumizi ya umeme nyumbani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma