99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mradi mkubwa wa kuzalisha umeme kwa maji wa Afrika Mashariki wakaribia kukamilika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 22, 2022

KIGALI - Kitengo cha Kuratibu Mpango wa Utekelezaji wa Programu Tanzu ya Maziwa ya Nile-Ikweta (NELSAP-CU) kimesema katika taarifa yake ya Jumamosi kuwa, ujenzi wa Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa Maji katika Maporomoko ya Rusumo umefikia asilimia 95 ya hatua ya utekelezaji kabla ya kuanza kutumika.

NELSAP-CU inasimamia mradi wa umeme kwa niaba ya serikali za Burundi, Rwanda, na Tanzania, ambazo ni wamiliki wa mradi huo.

Mradi huo wa kuzalisha umeme wa Megawati 80 katika maporomoko ya maji ya Rusumo uliopo kwenye mpaka wa Rusumo kati ya Rwanda na Tanzania unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu milioni moja katika eneo hilo la Afrika Mashariki utakapokamilika.

“Mradi wa kuzalisha Umeme kwa Maji katika Maporomoko ya Rusumo utakapokamilika utahimiza shughuli za kiuchumi, maendeleo ya sekta binafsi, na uwekezaji katika miundombinu kupitia kuboresha upatikanaji wa umeme katika eneo hilo,” amesema Ernest Nsabimana, Waziri wa Miundombinu wa Rwanda ambaye aliongoza baraza la mawaziri wa nchi za mradi huo siku ya Jumamosi kufanya ziara katika eneo hilo ili kutathmini maendeleo ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme.

Ziara hiyo ya ukaguzi pia ilihudhuriwa na Ibrahim Uwizeye, Waziri wa maji, nishati na madini wa Burundi, na January Yusuf Makamba, Waziri wa nishati wa Tanzania miongoni mwa wengine.

Taarifa hiyo imesema kuwa, ujumbe huo ulitathmini maendeleo ya eneo la ujenzi wa uzalishaji umeme, kituo cha umeme, na swichi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kazi za kihandishi na mitambo ya maji zimefikia asilimia 97 ya hatua ya kukamilika na sasa kazi inayoendelea ni ya urejeshaji na usafishaji wa eneo la mradi. Maendeleo ya kazi ya kielektroniki yamefikia takriban asilimia 93 huku kuta za mkondo wa chini za maji zikiwa zimekamilika.

Imeongeza kuwa, uwekaji wa muundo unaendelea na umepangwa kufungwa kikamilifu ifikapo mwisho wa mwaka huu.

Ziara hiyo ya mawaziri ilibaini kuwa usalama wa afya ya kijamii wa mradi huo ni utaratibu mzuri wa kuigwa kwenye miradi mingine ya baadaye ya kuzalisha umeme kwa maji na ubora wa kazi zote unabaki kuwa wa juu sana na wa kiwango cha kimataifa.

“Mpango wa kuwahamisha wakazi wa jirani na mradi unaendelea kukamilishwa,” imesema taarifa hiyo.

Kila moja ya nchi hizo tatu itapokea Megawati 26 zilizounganishwa moja kwa moja kwenye gridi ya taifa kupitia njia za kusambaza umeme, ambazo zinatarajiwa kunufaisha zaidi ya watu milioni moja katika nchi hizo tatu.

Ujenzi wa kituo hicho cha kuzalisha umeme kwa maji unafadhiliwa na Benki ya Dunia kwa dola milioni 340 za Kimarekani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha