99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Mabalozi wa nchi za kiislamu nchini China wasifu sera za China katika kushughulikia masuala ya mkoa wa Xinjiang

(CRI Online) Agosti 09, 2022

Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi 30 za kiislamu nchini China walitembelea mkoa wa Xinjiang kuanzia tarehe 1 hadi 5 mwezi huu.

Mabalozi hao wamesifu sera za serikali ya China katika kushughulikia masuala ya mkoa wa Xinjiang kwa kufuata msingi wa kutoa kipaumbele kwa wananchi, na wakisifu juhudi kubwa zilizofanywa na mafanikio mazuri yaliyopatikana mkoani Xinjiang katika maendeleo ya uchumi na mshikamano wa makabila.

Hayo yalisemwa na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin wakati akijulisha safari ya mabalozi hao kwenye mkoa wa Xinjiang.

Wang Wenbin amesema, wakati wa safari hiyo, mabalozi hao walijionea hali halisi kuhusu masikilizano kati ya makabila mbalimbali, uhuru wa kuabudu, na mafanikio yaliyopatikana katika kuondoa umaskini na kuleta ustawi wa vijiji katika mkoani Xinjiang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha