99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yasema ina matumaini ya kuweka biashara ya nje ndani ya viwango vinavyofaa Mwaka 2022

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2022

Picha iliyopigwa Mei 1, 2022 ikionyesha meli ya kontena ikitia nanga kwenye Kituo cha Kontena cha Qianwan huko Qingdao, Mkoa wa Shandong Mashariki mwa China. (Xinhua/Li Ziheng)

BEIJING – Wizara ya Biashara ya China Alhamisi wiki hii imesema China ina uhakika wa kuweka biashara yake ya nje katika kiwango kinachokubalika kwa mwaka mzima, na kutoa mchango zaidi katika misingi ya kiuchumi.

Thamani ya jumla ya uuzaji wa bidhaa na uagizaji wa bidhaa kutoka nje nchini China ilipanda kwa asilimia 9.6 kuliko mwaka jana mwezi uliopita ikiwa ni kiasi cha juu kuzidi asilimia 0.1 ya Mwezi Aprili, na kupata kasi ya kufufuka.

"Kuimarika huko kumekuja wakati ambapo uzalishaji kwenye biashara za nje umekuwa kipaumbele na hatua za kuhimiza ukuaji wa uchumi zilianza kutekelezwa," Msemaji wa wizara hiyo Shu Jueting amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Akibainisha kuwa hali ya kutokuwa na uhakika kama vile kuimarika kwa uchumi wa Dunia na matatizo yanayohusiana na gharama, minyororo ya ugavi na uchukuzi bado yapo, Shu amesema kuwa uratibu madhubuti wa udhibiti wa janga la UVIKO, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na hatua za kusaidia zitawezesha ukuaji wa biashara ya nje.

Kupunguza kodi na uwezeshaji wa biashara unaoletwa na mikataba ya biashara huria itakuwa na jukumu muhimu katika kukuza biashara ya nje, amesema Shu, akiongeza kuwa China ina kiasi kinachoongezeka cha washirika wa makubaliano ya biashara huria. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha