

Lugha Nyingine
McDonald's yatangaza kuondoka kutoka Russia na kuuza biashara yake nchini Russia
Alama ya McDonald's nchini Russia. (Picha kutoka Chinanews)
Shirika la habari la Ufaransa AP lilitoa Habari zikisema kuwa tarehe 16 kwa saa za huko, McDonald's, kampuni ya mnyororo wa mikahawa wa Marekani , imetangaza kwamba hatimaye imeamua kuondoka kutoka soko la Russia.
Habari zinasema, kampuni ya McDonald's ilisema katika taarifa kwamba kampuni hiyo "inatafuta kuuza migahawa yake yote ya McDonald nchini Russia kwa wanunuzi wenyeji," na kuongeza kuwa ingawa kampuni hiyo itaendelea kuhifadhi chapa yake ya biashara nchini Russia, lakini maduka yaliyopo sasa hayatatumia jina, alama, chapa au menyu za McDonald.
Machi 8 kabla ya hapo, McDonald's ilitangaza kwamba itafunga kwa muda maduka 850 nchini Russia, lakini itaendelea kutoa mishahara kwa wafanyikazi wake. Siku hiyo, Kampuni ya Starbucks na Kampuni ya Coca-Cola pia zilitangaza kusimamisha kwa muda biashara yao nchini Russia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma