99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Waziri wa mambo ya nje wa China aendesha mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa majirani wa Afghanistan

(CRI Online) April 02, 2022

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ameendesha mkutano wa tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani za Afghanistan, uliofanyika mkoani Anhui.

Kwenye mkutano Bw. Wang alisoma ujumbe kutoka kwa Rais Xi Jinping, na alitoa hotuba kwa niaba ya upande wa China. Amesema kwa sasa Afghanistan iko kwenye njia panda ya historia, na nchi jirani zimeanzisha mfumo wa uratibu wa ushirikiano, na kuweka maafikiano ya kisiasa ili kushirikiana kujibu mabadiliko kwenye hali ya Afghanistan.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zilizohudhuria kwenye mkutano huo wamemshukuru Rais Xi kwa ujumbe aliotoa kwa mkutano huo, ambao umetajwa kuwa umeongeza msukumo wa ushirikiano kati ya nchi jirani za Afghanistan. Pia wamepongeza mchango wa China kuzileta pamoja nchi hizo na kuunga mkono ujenzi mpya wa amani wa Afghanistan.

(Picha inatoka tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha