99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China ina imani ya kufikia lengo la ukuaji wa uchumi katika mwaka licha ya changamoto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2022

Picha iliyopigwa Desemba 1 2021 inaonyesha kituo cha kontena huko Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu nchini China. (Picha na Si Wei/Xinhua)

BEIJING - China imeeleza matumaini kwamba ina mazingira muhimu na wezeshi ya kufikia malengo ya mwaka huu ya ongezeko la uchumi kwa kufanya kazi kwa bidii licha ya kuwepo kwa muda mrefu janga la UVIKO-19 na changamoto zinazoongezeka.

Katika ripoti mpya ya kazi ya serikali, China iliweka lengo lake la ukuaji wa uchumi kwa 2022 katika kiwango cha karibu asilimia 5.5, na kusababisha baadhi ya watu kuhoji kama lengo hilo "linazidi kuwa lisilowezekana" kwani nchi hiyo inazingatia sera yake ya “Maambukizi sifuri ya UVIKO”.

Hata hivyo, kwa mujibu wa wachambuzi, mbinu hiyo madhubuti ya kukabiliana na UVIKO-19 imeonekana kuwa nzuri siyo tu katika kulinda afya ya umma, lakini pia katika hali ya kiuchumi, kwani faida kutoka kwa uzalishaji na ununuzi na utumiaji wa kawaida wa bidhaa inazidi gharama za kudhibiti janga.

Fu Linghui, Msemaji wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) amesema Jumanne wiki hii kwamba, sera za kuratibu udhibiti wa UVIKO-19 na maendeleo ya kiuchumi zimezaa matunda, huku uchumi wa China ukifufuka kwa kasi nzuri katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, na kuashiria mwanzo mzuri wa Mwaka 2022.

Viashiria vya ukuaji wa uchumi nchini China viliimarika katika kipindi cha Januari hadi Februari mwaka huu, huku viashirio vikuu vya uzalishaji na mahitaji vikikua kwa kasi nzuri ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2021.

Kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu, pato la China la ongezeko la thamani la viwanda na mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi yameongezeka kwa asilimia 7.5 na 6.7 kuliko mwaka jana, ikiwa ni kiwango cha juu kwa asilimia 3.2 na 5 kuliko ilivyokuwa Mwezi Desemba mwaka jana.

Fu amesema, viashirio katika nyanja mbalimbali vilionyesha dalili chanya huku sera za kuhakikisha ukuaji thabiti wa uchumi zimeanza kutekelezwa.

Katika kipindi cha miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa mali zisizohamishika wa China ulipanda kwa asilimia 12.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita, huku uwekezaji katika sekta za ujenzi wa nyumba ukiongezeka kwa asilimia 3.7.

Kwa mujibu wa NBS, likizo ya Sikukuu ya Spring na Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022 ilichochea kukukua kwa sekta ya huduma, ikiwa ni pamoja na migahawa, usafiri wa reli na anga, na shughuli za kitamaduni na burudani.

Fu amesema kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi inazidi kuimarika, lakini akaonya kuwa bado kuna hali ya kutokuwa na uhakika inayojitokeza kama vile kupanda kwa bei za bidhaa za kimataifa na mahusiano tete ya kimkakati na kijiografia ambayo yana athari katika soko la fedha la kimataifa.

Uchumi wa China unabaki kwenye njia sahihi ya kufufuka, kwa uthabiti na uwezo mkubwa, amesema Fu, na kuongeza kuwa nchi hiyo imechukua nafasi ya kuongoza katika ukuaji wa uchumi huku kukiwa na changamoto za janga duniani katika miaka miwili iliyopita.

"Utendaji wa kiuchumi katika miezi miwili ya kwanza utaimarisha imani yetu katika kutimiza ukuaji wa pato la taifa kwa asilimia 5.5 katika Mwaka 2022," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha