99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

China yafaulu kurusha satelaiti E ya Fengyun No.3

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 06, 2021

(Picha inatoka Tovuti ya Shirika la Habari la China Xinhua.)

Julai 5, saa moja na ishirini na nane, China imefaulu kurusha satelaiti E ya Fengyun No.3 kwa maroketi ya C ya Changzheng No.4 hadi kwenye obiti iliyopangiwa kwenye anga ya juu kutoka kituo cha kurusha satelaiti ya Jiuquan. Kazi hii ya kurusha satelaiti imefanikiwa vizuri.

Kazi hii ni mara ya 377 ya kurushwa kwa maroketi ya Changzheng ya kubeba satelaiti.

Satelaiti hii, ambayo ni satelaiti ya kwanza ya ufuatiliaji wa hali ya hewa ya matumizi ya kiumma kwenye obiti ya alfajiri/jioni duniani, itafanya kazi kwa kushirikiana na satelaiti C na satelaiti D ya Fengyun No.3, ikifanya China iwe nchi ya kipekee yenye uwezo wa kufuatilia hali ya hewa kwa kupitia mtandao wa satelaiti za obiti tatu: obiti ya alfajiri/jioni, obiti ya asubuhi na obiti ya mchana.

Wataalam wanakadiria kuwa, mtandao huo wa satelaiti huenda utainua kiwango cha utabiri sahihi wa hali ya hewa wa kila nusutufe ya dunia kwa asilimia 2 hadi asilimia 3, na kuinua kiwango cha utabiri sahihi wa hali ya hewa cha kibara kwa asilimia 2 hadi asilimia 10.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha