Miaka 20 ya wazo la “milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha”: Safari ya Chanzo cha Mito Mitatu
Katika eneo la kusini mkoani Qinghai, kaskazini magharibi mwa China, eneo ambalo ni kiini cha Uwanda wa Juu wa Qinghai-Tibet, Mto Yangtze, Mto Manjano na Mto Lancang inaanza safari zake za kuelekea bahari. Hili ni eneo la chanzo cha mito hiyo mitatu linalojulikana kuwa ni “mnara wa maji” wa China.
Mnamo mwezi Juni, 2021, rais Xi Jinping wa China alipofanya ukaguzi mkoani Qinghai alisisitiza “mito ya maji safi na milima ya kijani ndiyo inayoleta utajiri”, akisisitiza pia kuhifadhi mazingira ya mkoa wa Qinghai ni moja ya majukumu muhimu ya kwanza ya China, na kutoa wito wa kufanya uhifadhi wenye ufanisi katika mazingira haya ya ikolojia ya “ncha ya tatu’ ya dunia.
Oktoba 12, 2021, Bustani ya Kitaifa ya Chanzo cha Mito Mitatu iliorodheshwa kuwa moja ya bustani za kitaifa za China, ikiwa na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 190,700. Ndani ya bustani hiyo linahifadhiwa eneo kubwa la mfumo wa ikolojia wa mlima mrefu ambao haujaharibiwa, likiwa ni eneo kubwa zaidi la mfumo wa ardhi oevu ya Uwanda wa Juu lililo la mwinuko wa juu zaidi kutoka usawa wa bahari duniani.
Baada ya kufanya majaribio na ujenzi katika miaka mingi iliyopita, Bustani ya kitaifa ya chanzo cha mito mitatu imefikia hali ya kuunganishwa vizuri kwa uhifadhi wa ikolojia, maendeleo yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira, na uboreshaji wa maisha ya watu. Hivi sasa eneo hilo lina mazingira mazuri ya milima ya kijani na mito yenye maji safi, na ustawi wa mimea na viumbe, huku wakazi wa huko wakiishi maisha na kufanya kazi katika hali ya amani na furaha.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma