99久久国产综合色|国产精品,日韩AV一级特黄无码人妻,91在线视频无码,国产网站久章草在线视频

Miaka 20 ya wazo la “milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha”: Kuziwezesha bahari buluu na pwani kuwa dhahabu na fedha

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 02, 2025

Mwaka huu ni mwaka wa 20 tangu kutolewa kwa wazo la "milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha".

Milima ya kijani na maji safi ni dhahabu na fedha, hivyo bahari buluu na pwani pia inaweza kuwa dhahabu na fedha. Milima ya kijani na maji safi si kama tu ni hazina za kiekolojia za kuwalea viumbe vyote, bali pia ni chanzo cha uchumi wa kuleta mali muhimu. Kulinda hali ya ikolojia ndiyo kulinda "mali ya mazingira ya asili", kuhuisha vizuri mazingira ya ikolojia kutaweza kuchochea juhudi za kuleta "mali za kijani".

Ukifika kijiji cha Aojiao cha Kisiwa cha Dongshan, mara utakabiliwa na upepo wenye chumvi na unyevunyevu kutoka baharini. Meli mojamoja zinapangwa kwenye safu ndani ya bandari ya ghuba ya Kijiji cha Aojiao, zikingoja honi kutoa sauti ya kufunga safari ya kwenda baharini. Kwenye gati lililoko karibu, watalii kutoka sehemu mbalimbali nchini pia wamesimama huko kungoja kwenda kutalii kwenye bahari, ambapo mabanda ya kuuza samaki pia yameanza kazi zao, na yako tayari kuwakaribisha wateja kutoka pande mbalimbali.

Kijiji cha Aojiao kiko kwenye pembe moja la kusini mashariki mwa Kisiwa cha Dongshan, pande tatu zake zinazunguka bahari buluu. Watu wa Kijiji cha Aojiao wakitegemea maliasili ya baharini kuishi maisha yenye ustawi siku hadi siku. Hasa tokea Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa kijiji hicho wanajitahidi kutumia vya kutosha maliasili za baharini, wakiendeleza shughuli za uvuvi, ufugaji wa samaki, utengenezaji wa mazao ya samaki, ukuaji wa biashara mtandaoni na shughuli za utalii kijijini, kijiji hiki kilichokuwa kijiji kidogo cha uvuvi kimefuata njia mpya ya kujenga "mazingira mazuri ya asili ya ikolojia" na "kuleta ustawi kwa raia", na kutimiza lengo la "bahari buluu na pwani pia ni dhahabu na fedha".

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha