

Lugha Nyingine
Mchumi wa Mauritania atwaa ukurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
Mchumi wa Mauritania Bw. Sidi Ould Tah ameapishwa kuwa mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwenye makao makuu ya benki hiyo mjini Abidjan, Cote d'Ivoire.
Sherehe ya kuapishwa kwake ilihudhuriwa na Rais Alassane Ouattara wa Cote d'Ivoire, Rais Mohamed Ghazouani wa Mauritania, na wajumbe wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Bw. Ould Tah alichaguliwa tarehe 29 Mei kuwa mkurugenzi wa tisa wa benki hiyo, na kupata zaidi ya asilimia 76 ya kura, idadi kubwa zaidi ya kura za muhula wa kwanza katika historia ya benki hiyo.
Bw. Ould Tah amechaguliwa kwa muhula wa miaka mitano, na ametaja nguzo nne za kimkakati katika kipindi chake, kuwa ni kufungua raslimali za kifedha za Afrika, kurekebisha na kuimarisha mamlaka ya kifedha ya Afrika, kufanya demografia ya Afrika kuwa na manufaa, na kujenga miundombinu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma